loader
Bashe atoa maagizo miradi ya umwagiliaji

Bashe atoa maagizo miradi ya umwagiliaji

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe ameitaka Menejimenti ya Tume ya Umwagiliaji nchini, kuwakutanisha wakandarasi walioshinda zabuni ya ujenzi wa mabwawa kwenye miradi ya umwagiliaji na wabunge wa majimbo ambayo miradi hiyo inaenda kutekelezwa, ili ieleweke vyema kwa wabunge na waisimamie kikamilifu.

Bashe ametoa agizo hilo wakati alipokutana na watendaji na Bodi ya Tume hiyo leo, ambapo amesema iwapo wabunge wakishirikishwa watasaidia usimamizi wa miradi hiyo na itatekelezwa kwa ufanisi mkubwa.

Amesema serikali inataka miradi ya umwagiliaji ifanikishe utekelezwaji wa sera ya kilimo cha umwagiliaji, ili kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua, hivyo lazima wakandarasi wasimamiwe kikamilifu.

Pia ameitaka bodi hiyo kusimamia ukusanyaji mapato yanayotokana na miradi ya umwagiliaji nchi nzima.

Bashe amewataka wakandarasi kutekeleza miradi waliyopewa kwa  ufanisi na kuwa atakayefanya kazi chini ya kiwango hatoruhusiwa kufanya kazi yoyote ya ukandarasi hapa nchini.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/b9e9d7c154ea38c07522bbfcf2447a64.jpg

WIZARA ya Nishati imesema Benki ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi