loader
Chaurembo Palasa Rais ngumi za kulipwa

Chaurembo Palasa Rais ngumi za kulipwa

BONDIA wa zamani nchini, Chaurembo Palasa amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC).

Palasa ametwaa wadhifa huo leo Jumamosi Mei 14, 2022, baada ya kupata kura 11 na kuwashinda wapinzani wake wake Bakari Songoro aliyepata kura 10 na Chatta Michael ambaye hakupata kura.

Wengine walioshinda upande wa ujumbe katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Baraza la Michezo nchini (BMT), ni Ibrahim Kamwe na Amos Mwamakula, wakati Elius Mlundwa alichaguliwa kuwa Mhazini.

Uchaguzi huo wa leo ilikuwa kujaza nafasi zilizopo wazi kutokana na sababu mbalimbali ndani ya TPBRC, ikiwemo waliokuwa wakizishikilia kujiuzulu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d67ca4278ef22b294b6c274ee5722faf.jpg

VINARA wa Ligi Kuu, Yanga SC, wanahitaji ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi