loader
Fatma Karume  ataka serikali 3

Fatma Karume ataka serikali 3

WAKILI wa Kujitegemea, Fatma Karume ameshauri uwepo mfumo wa muungano wa serikali tatu tofauti na uliopo hivi wa serikali mbili huku akipendekeza kuanza haraka mchakato wa kupatikana katiba mpya.

Fatma ambaye ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akitoa mapendekezo yake mbele ya Kikosi Kazi cha Rais Samia Suluhu Hassan ambacho ni maalumu kwa ajili ya kukusanya maoni kuhusu demokrasia na vyama vya siasa. Katika mapendekezo yake alisema anahitaji uwepo wa serikali tatu kwa sababu maoni ya Watanzania wengi kupitia tume ya Jaji Warioba walitaka hivyo licha ya kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakikutaka.

“Kutokana na mitazamo hiyo kuna mgongano kati ya wanasiasa wa CCM na watu wa UKAWA na maoni ya wananchi wenyewe wanaotaka serikali tatu, CCM wanadhani tukiwa na muundo wa Serikali tatu pengine nchi itapasuka,” alisema Fatma.

Alisema inawezekana watu wa pande zote hawataki muungano lakini ni vyema kuwasikiliza wananchi wanataka kitu gani? Ni muhimu kuangalia namna ya kuweka mchakato ambao hautalipeleka taifa kubaya.

“Ni vizuri kuweka mchakato huo badala ya kuendelea kuwaita wahaini wanaoonekana kupinga muungano uliopo na hasa kwa sasa kuna Watanzania wengi ambao inawezekana hawataki muungano wapewe nafasi ya kusikilizwa,” alisisitiza.

Aidha, Mwanasheria huyo alipendekeza pia yapunguzwe madaraka ya Rais ili kumfanya asiwe kama sultani hasa kwa kumpa majukumu ya kufanya teuzi mbalimbali zikiwemo za majaji na wakuu wa mikoa.

“Rais asiwe na uwezo wa kuchagua Kamanda wa Jeshi la Polisi (IGP) na watendaji wa kudumu, kwani nafasi hizo zinatakiwa zizingatie weledi kwa sababu wanatoa huduma kwa jamii badala ya siasa kama ilivyo sasa,” alisema.

Fatma alisema ni lazima Katiba mpya ipatikane ili kumpunguzia Rais hayo madaraka na ili ipatikane katiba yenye kulinda maslahi ya wananchi ni lazima iundwe kamati ya wataalamu wabobevu wa sheria na katiba na si wanasiasa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/017b07b8e7b45252a5e3ea3f5c0bcf35.jpg

WAKALA wa Maji na Usafi wa ...

foto
Mwandishi: OSCAR JOB

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi