loader
Wastaafu wahadharishwa  matapeli mitandaoni

Wastaafu wahadharishwa matapeli mitandaoni

WIZARA ya Fedha na Mipango imewahadharisha wastaafu dhidi ya matapeli walioibuka mitandaoni wakidai ni madalali wa kuwasaidia kupata mafao yao badala yake wafi ke kuhudumiwa katika ofi si za hazina ndogo mikoani au makao makuu ya wizara jijini Dodoma.

Mhasibu Mkuu wa Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango, Leonard Mkude alitoa kauli hiyo jana jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Hazina.

“Wameibuka matapeli mitandaoni wanaodai kusaidia wastaafu kupata mafao yao, wanatakiwa kujihadhari kwani hazina haina madalali wanaosaidia kupata mafao yao,” alisema.

Mkude alisema kutokana na kuibuka kwa matapeli hao mitandaoni, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inashughulikia jambo hilo kuwachukulia hatua. Alifafanua kwamba wizara inatumia ofisi zake zilizopo katika kila mkoa na haina madalali wa kusaidia wastaafu kupata mafao yao hivyo hawapaswi kutoa chochote ili kupata huduma.

Kuhusu malalamiko kwamba Hazina inachelewesha mafao ya wastaafu, Mkude alisema hawacheleweshi bali hutoa mapema maadam taratibu zote ziwe zimekamilika.

Alisema mfano mzuri ni wastaafu kutoka majeshi, majaji na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) waliohamishiwa hazina, wamekuwa wakipata mafao yao kwa haraka.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Jenifa Omolo alitoa wito kwa wafanyakazi wa wizara hiyo nchini kutoa huduma bora na kwa weledi kwa watumishi wote nchini.

Katika mkutano huo wa baraza la wafanyakazi wa Hazina, uliolenga kuangalia malalamiko ya wafanyakazi waliyotoa mwaka jana pamoja na utekelezaji wa bajeti ya 2020/2021 pamoja na kutoa mapendekezo ya mapato, makadirio na matumizi ya bajeti ya 2020/2023, wizara imetekeleza mahitaji ya wafanyakazi katika bajeti iliyopita kwa asilimia 90.

Miongoni mwa malalamiko yaliyojitokeza katika bajeti iliyopita ni uhaba na ubovu wa ofisi za wizara ambayo tayari wizara imetekeleza hilo kwa kuendelea kujenga ofisi za hazina ndogo kila mkoa na kuzifanyia ukarabati zilizochakaa.

Kuhusu ombi la maslahi bora, Omolo alisema kwa kuwa serikali imeahidi kupandisha mishahara wafanyakazi wote, wizara inaiachia. Omolo alitoa wito kwa wafanyakazi wa Hazina nchini kufanya kazi kwa bidii na kwa weledi katika kuhudumia wananchi kwenye masuala ya fedha kupitia hazina ndogo ambazo zipo katika kila mkoa nchini.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a9f0ec24b6246211e2df96678dd3e501.jpg

MBUNGE wa Kigamboni, Dk Fausitine Ndugulile (CCM) ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi