loader
Watu milioni 2.5 kuajiriwa sekta ya nyuki

Watu milioni 2.5 kuajiriwa sekta ya nyuki

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya Siku ya Nyuki duniani ambayo kitaifa yatafanyika katika Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Mei 21, mwaka huu.

Lengo la maadhimisho ni kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu umuhimu wa nyuki katika maisha ya kila siku ya mwanadamu na mazingira yake.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana alitoa wito huo kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari jana. Alisema chimbuko la maadhimisho hayo ni azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa la De- semba 20, 2017.

“Kufuatia azimio hilo, kila nchi ina jukumu la kuadhimisha siku hiyo kuendana na mazingira yake ili kuendelea kujenga uelewa kwa jamii juu ya umuhimu wa mdudu nyuki na hii ndiyo sababu, sisi kama nchi, tunaungana na dunia kufanya maadhimisho haya kwa mara ya tatu tangu yalipoanzishwa miaka mitano iliyopita,” alisema.

Alitaja manufaa ya nyuki ni pamoja na kujipatia chakula na dawa, fedha za ndani na kigeni, ajira zaidi ya watu milioni mbili katika mnyororo mzima wa thamani itokanayo na sekta ya ufugaji wa nyuki.

Alisema Wizara ina mikakati ya kuhakikisha sekta ya nyuki inaajiri zaidi ya watu milioni 2.5 ifikapo mwaka 2031. Kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Nyuki wamehusika: Harakati za kujikwamua upya zisisahau nyuki’. Kwa upande wa kaulimbiu ya kitaifa mwaka huu ni ‘Nyuki ni uchumi: Tuwalinde na Kuhifadhi mazingira yao’.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/a52215dcc5b275fa2ce198b7ead6bdc7.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan, ametajwa kuwa miongoni ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi