loader
Kaze: Msiiwaze Simba

Kaze: Msiiwaze Simba

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amewataka wachezaji wa timu hiyo kuweka mawazo yao kwenye mechi za Ligi Kuu zinazowakabili badala ya kufikiria mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Simba.

Nusu fainali ya Kombe la FA, itazikutanisha timu hizo Mei 28 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kila timu imepania kutaka kushinda mchezo huo ili kucheza fainali.

Akizungumza na HabariLEO jana, kocha huyo msaidizi alisema mataji yote mawili yapo katika malengo yao lakini kwa sasa wanapaswa kuweka nguvu zao kwenye mechi mbili za ligi zinazowakabili ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutangaza ubingwa kuliko mchezo wa Simba.

“Mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba tunaupa uzito mkubwa lakini kwa sasa wachezaji hawapaswi kuufikiria sababu tuna mechi mbili za Ligi Kuu kabla ya mchezo huo na tunapaswa kushinda ili kujiweka karibu na malengo yetu na baada ya hapo ndio tutaanza kufikiria namna ya kuikabili Simba,” alisema Kaze.

Alisema ingawa wanaongoza kwa tofauti ya pointi 11 kwenye ligi lakini hicho hakipaswi kuwa kigezo cha kujiamini na kushindwa kuzipa umuhimu mechi zilizobaki kwani pointi walizokuwa nazo bado hazijatosha kuwapa ubingwa.

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi