loader
Watoto 846,733 kupatiwa chanjo ya polio Mwanza

Watoto 846,733 kupatiwa chanjo ya polio Mwanza

ZAIDI ya watoto 846,733 kutoka mkoa wa Mwanza, wanatarajia kupata chanjo ya  ugonjwa wa polio.

Hayo yamesemwa leo na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Thomas Rutachunzibwa, wakati wa uzinduzi wa chanjo ya polio katika kituo cha afya cha Nakatunguru Wilaya ya Ukerewe.

Dk Rutachunzibwa,  amesema chanzo hiyo imeanza leo na itaendelea hadi Mei 21mwaka huu.

"Tumejipanga  kutoa chanjo vituo 355, ambapo jumla ya watoa huduma 6,909 wamepata mafunzo kwa ajili ya kutoa huduma hiyo, " amesema Dk. Rutachunzibwa.

Amesema Wilaya ya Ukerewe kuna watoto 108,937, wenye umri wa chini ya miaka mitano,  ambao wote watapewa chanjo ya matone ya polio.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel, amesema wazazi waoneshe ushirikiano kwa watoa huduma ya chanjo, ili watoto  waweze kupata chanzo hiyo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/3c82325bf5b4d9f589f148870974fed1.jpg

WIZARA ya Afya inaendelea na ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi