loader
Rais Samia ataka ufugaji wa kisasa Tabora

Rais Samia ataka ufugaji wa kisasa Tabora

RAIS Samia Suluhu Hassam, ameiagiza Wizara ya Ardhi itumie vyema ardhi kwa kupanga matumizi bora itumike kama ilivyokusudiwa.

Akizungumza leo Mei 18, 2022 katika ufunguzi wa barabara ya Tabora, Koga – Mpanda KM 342.9, Rais Samia amewataka wafugaji kubadilika na kuwa na mifugo yenye tija, badala ya kuona fahari kuwa na mifugo mingi isiyowaletea tija wala maendeleo.

“Si wakati wa kuona fahari, niwaombe Wanyemwezi na Wasukuma wenzangu huu si wakati wa kukaa na ng'ombe wengi ambao hawakuletei faida, kukaa na ng'ombe wengi wasio na faida si zama hizi, kwani wanasababisha kuhitaji ardhi kubwa na kuharibu vyanzo vya maji na kuharibu mazingira pamoja na kukosekana mvua kutokana na ukataji miti.Tubadilike,” amesema.

Amewataka  Wizara ya Ardhi na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Taasisis ya Misitu (TFS)  kukaa na kupanga  matumizi mazuri ya ardhi, ili kilimo kiwepo, uvuvi uwepo na ufugaji uwepo mvua ipatikane na maendeleo yapatikane bila kuharibu mazingira.

“Nina taarifa za wavuvi  kwenye mto Ugala kuwa maofisa wanatengeneza mazingira ya rushwa kwa kuwazuia watu kuvua ili wale wanaotoa fedha ndio wanaruhusiwa kuvua, naomba wizara husika iliangalie suala hilo ipasavyo,” amesema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8010be3201489c72eec5b151d0e5e766.jpg

MKURUNGENZI wa Kampuni ya Prosperity ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi