loader
Geita yaipeleka Simba Kirumba

Geita yaipeleka Simba Kirumba

TIMU ya Geita Gold imeuhamishia mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba kwenda Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza  badala ya Nyankumbu, ili kutoa fursa kwa mashabiki wengi kuushuhudia mtanange huo.

Mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa  Mei  22, awali ulitakiwa kuchezwa kwenye Uwanja Nyankumbu, ambao wamekuwa wakiutumia katika baadhi ya michezo  yake ya nyumbani.

Huu utakuwa wa pili kuzikutanisha timu hizo msimu huu baada ya  ule wa awali uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Geita Gold kukubali kichapo cha 1-0.

Akizungumza jana Mtendaji Mkuu wa Geita Gold, Simon Shija alisema kuwa wamefanya hivyo kuwatoa hofu mashabiki wao baada ya taarifa zisizo rasmi kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii, hivyo  mchezo huo utachezwa CCM Kirumba  kuanzia saa 10:00 jioni.

“Tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi  uwanjani ili kuipa sapoti  timu yao iweze kupata ushindi  na kuondoka na pointi tatu kwenye mchezo huo,” alisema Shija.

Alisema kuwa huo ni mchezo muhimu kwao kutokana na malengo waliyo nayo, ambayo ni kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa mwakani.

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi