loader
Mambo safi miradi ya maji Pangani

Mambo safi miradi ya maji Pangani

WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini mkoani Tanga (RUWASA), umesaini mkataba wa ujenzi wa miradi miwili ya maji, ambayo itatekelezwa wilayani Pangani yenye thamani ya Sh Bil 1.5.

Utiaji saini mikataba hiyo ulifanyika mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Ghaibu Lingo, pamoja na wakandarasi watakaohusika na ujenzi huo.

Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga, Upendo Lugongo amesema miradi hiyo inatekelezwa katika Kata za Kipumbwi na Masaika, itaweza kusaidia kumaliza changamoto ya ukosefu wa huduma kwenye maeneo hayo.

"Mradi wa maji Kipumbwi unatekelezwa na mkandarasi M/s Matrix Technology Company Ltd una gharama ya Sh Mil 703, huku mradi wa Mronzo uliopo kata ya Masaika unatarajia kutumia Sh mil 825.5 na utatekelezwa na Mkandarasi KGG investment,"amesema Lugongo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Ghaibu Lingo, aliipongeza serikali kwa kuja na mpango wa ujenzi wa miradi ya maji kwa kutumia wakandarasi wazawa, kwani imeweza kuleta matokeo ya haraka na wananchi wengi wamenufaika na fursa ya ajira.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9c0c6c7d625728ed4c627ef36f14194c.jpg

MKURUNGENZI wa Kampuni ya Prosperity ...

foto
Mwandishi: Amina Omari, Pangani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi