loader
Tamisemi yazionya halmashauri mikopo

Tamisemi yazionya halmashauri mikopo

OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imezionya halmashauri kuhusu mikopo kwenye vikundi hewa na kwa wasio walengwa.

Pia jana Waziri wa wizara hiyo, Innocent Bashungwa aliagiza wakurugenzi wa majiji, manispaa na miji ambayo inakusanya mapato zaidi ya Sh bilioni 5 watenge na kutoa fedha asilimia 10 kwa ajili ya kuimarisha barabara za mitaa.

Bashungwa alisema hayo Dodoma jana wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Alisema suala la fedha za mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi imekuwa ni hoja ya mara kwa mara ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na Bunge na akasema  baada mafunzo hayo hataki kusikia vikundi hewa au fedha za mikopo zinakwenda kwa wasio walengwa.

Bashungwa alisisema waliopewa mafunzo hayo wanapaswa kufuatilia mikopo kwa vikundi ili kuwe na tija.

Bashungwa aliagiza kusimamiaji madhubuti wa marejesho ya mikopo hiyo ili fedha hizo zitumike na vikundi vingine.

Alimuagiza Katibu Mkuu, Profesa Riziki Shemdoe aimarishe sekretarieti za mikoa na za wilaya kwa kuangalia uwezo na udhaifu ili kuimarisha usimamizi wa miradi ya maendeleo.

Pia alimuagiza Shemdoe aimarishe mifumo kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kudhibiti upotevu wa mapato katika halmashauri.

Aidha alimuelekeza Katibu Mkuu wa wizara hiyo asimamie mwongozo unaotaka halmashauri zinazokusanya zaidi ya Sh bilioni itenge asilimia 10 kwa ajili ya kutengeneza barabara za mitaa.

"Suala hili siyo hiyari ni lazima, hivyo mwongozo kwa halmashauri za aina hizi kutenga asilimia 10 usimamiwe vizuri ili kodi wanayokisanya wanakwenda kuwahudumia wananchi," alisema Bashungwa.

Shemdoe alisema Ofisi ya Rais-Tamisemi imekuja na mfumo wa kieletroniki ikiwa kutafuta njia bora ya kuhakikisha fedha za asilimia 10 kwa vikundi zinakusanywa, zinatumika na zinarejeshwa.

Mkuu wa Idara ya Uhusiano Benki ya NMB Ofisi Ndogo ya Dodoma, Vicky Bushumbo alisema benki ilisaidia Sh milioni 130 kuuboresha mfumo huo na Sh milioni 10 kwa ajili ya mafunzo.

"Kumekuwapo na malalamiko ya mikopo hii ya asilimia 10 kwamba hairejeshwi kwa kiwango kinachotakiwa, sisi tumejiandaa na kwa kuanzia tumeweza kuweka kanzidata ya vikundi zaidi ya 40,000"alisema Bushumbo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/24cdb960c6e3d302b46ac3af96537224.jpg

MKURUNGENZI wa Kampuni ya Prosperity ...

foto
Mwandishi: Anastasia Anyimike, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi