loader
Mbarawa ataja mafanikio, changamoto 11

Mbarawa ataja mafanikio, changamoto 11

WIZARA ya Ujenzi na Uchukuzi imetaja mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ikiwa ni pamoja na serikali kutoa fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati yakiwemo madaraja.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo, bungeni jana, Profesa Makame Mbarawa aliyataja madaraja hayo kuwa ni Daraja la J.P. Magufuli lililopo Kigongo-Busisi mkoani Mwanza, daraja la Wami mkoani Pwani na Daraja la Tanzanite Dar es Salaam ambalo limekamilika.

Alisema fedha hizo pia zilifanikisha ujenzi wa nyumba za makazi kwa ajili ya familia 644 za wakazi wa Magomeni Kota, ujenzi unaoendelea wa barabara ya mzunguko wa nje yenye urefu wa kilometa 112.3 jijini Dodoma na mradi wa mabasi ya mwendokasi awamu ya tatu mkoa wa Dar es Salaam wenye urefu wa kilometa 23.

Kwa mujibu wa Profesa Mbarawa fedha hizo pia zilipelekwa kwenye ujenzi wa barabara ya Tanga-Saadani-Bagamoyo kilometa 256, Malagarasi–Ilunde–Uvinza kilometa 51.1, Bugene-Kasulo (Benaco)-Kumunazi kilometa 128.5 na sehemu ya Bugene-Burigi Chato National Park kilometa 60.

Pia alisema miradi mingine 22 ya barabara imepata kibali cha kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami wakati barabara nyingine ziko katika hatua ya manunuzi ya kupata makandarasi ikiwemo ya TAMCO–Vikawe–Mapinga kilometa 24.

Kuhusu usafiri wa reli, Profesa Mbarawa alisema serikali imeendelea na ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kwa awamu mbili ikiwemo awamu ya kwanza iliyogawanyika katika vipande vitano kati ya Dar es Salaam na Mwanza ambavyo ujenzi wake upo katika hatua mbalimbali.

 Pia alisema serikali imeanza utekelezaji wa ujenzi wa SGR awamu ya pili kati ya Tabora na Kigoma ambapo fedha za utekelezaji wa mradi huo zimeanza kutengwa katika mwaka wa fedha 2022/2023.

"Serikali ya Awamu ya Sita imeonesha dhamira ya dhati ya kuboresha viwanja vya ndege ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za usafiri na usafirishaji kwa njia ya anga;imeendelea kuboresha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kukamilisha ujenzi wa gati la kushusha magari na kuboresha gati namba moja hadi saba,"alisema Profesa Mbarawa.

Alisema pamoja na mafanikio hayoi wizara hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwamo ya ufinyu wa bajeti,  uvamizi wa maeneo ya hifadhi ya barabara na ushiriki hafifu wa makandarasi wa ndani katika utekelezaji wa miradi mikubwa.

Changamoto nyingine alizozitaja ni mahitaji ya fedha za matengenezo ya barabara, uharibifu wa barabara kutokana na uzidishaji wa uzito wa mizigo, ugonjwa wa Covid-19 ambao umeathiri sekta ya uchukukuzi, uhaba wa wataalamu katika sekta ya uchukuzi, uvamizi, uharibifu na wizi wa miundombinu ya reli, mabadiliko ya hali ya hewa na upungufu wa taa za kuongozea ndege katika viwanja vya ndege.

Profesa Mbarawa aliliomba Bunge liidhinishie Sh trilioni 3.9 kwa ajili ya bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 na kwamba, kati ya fedha hizo, Sh trilioni 1.5 ni kwa ajili ya sekta ya ujenzi na Sh trilioni 2.4 kwa ajili ya sekta ya uchukuzi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/60ce4b5b222e32caa815e5e06185c32f.jpg

WIZARA ya Afya inaendelea na ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi