loader
Mwingine aongezwa kesi ya Kisena na wenzake

Mwingine aongezwa kesi ya Kisena na wenzake

MKURUGENZI wa Kampuni ya Maxicom Africa, Juma Furaji ameunganishwa katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (BRT), Robert Kisena na wenzake.

Mkurugenzi huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Issaya.

Katika kesi hiyo upande wa mashtaka uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali waandamizi, Ester Martin, Jackine Nyantori na Mwendesha mashtaka kutoka Takukuru, Imani Nitume.

Akisoma mashtaka hayo, Nitume alidai mshtakiwa huyo aliunganishwa katika mashtaka sita kati ya 22 yanayowakabili, manne yakiwa ni ya utakatishaji, moja la kuongoza genge la uhalifu na moja la kuisababishia mamlaka hasara.

Katika mashtaka ya kwanza mshtakiwa huyo na wenzake wanakabiliwa na mashtaka la kuongoza genge la uhalifu ambapo ilidaiwa kati ya Agosti mosi, 2015 na Desemba, 2015 waliongoza genge la uhalifu na kujipatia Sh 4,505,125,000 katika Benki ya NMB Makao Makuu.

Katika mashtaka ya utakatishaji ambayo ni la 11, 14, 16 na 19 mshtakiwa huyo alidaiwa Novemba 18, 2015 katika Mkoa wa Dar es Saalaam kwa nia ovu alihamisha Sh 1,100,000,000 kutoka katika akaunti ya Maxcom Africa iliyopo Benki ya International Commercial kwenda kwenye akaunti ya Robert Kisena iliyopo katika benki hiyo.

Iliendelea kudaiwa kuwa Novemba 19, 2015 alihamisha tena Sh 1,200,000,000 kwenda katika akaunti ya Kisena na katika tarehe hiyo pia alihamisha Sh 829,500,000 kwa mara nyingine Novemba 27, 2022 alihamisha Sh 1,100,000,000 kwenda kwenye akaunti ya Kisena vyote hivyo akijua ni zao la makosa ya kughushi.

Na katika mashtaka mengine ya kuisababishia mamlaka hasara ilidaiwa washtakiwa wote kwa pamoja waliisababishia UDART hasara ya Sh 4,505,125,000.

Baada ya kusomewa mashtaka Wakili Martin alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wako katika utaratibu wa kuandaa maelezo ya mashahidi na aliomba tarehe nyingine. Hakimu Issaya aliahirisha kesi hadi Juni 6, 2022.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/41ec8f5d67d9908c588a0d0e0b93bb26.jpg

WIZARA ya Afya inaendelea na ...

foto
Mwandishi: Anna Mwikola

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi