loader
NMB Teleza Kidijitali yafika Arusha

NMB Teleza Kidijitali yafika Arusha

BENKI ya NMB katika kuendeleza ubunifu na kuwarahisishia huduma wateja wake, imekuja na mfumo mpya wa malipo ya huduma wa kidijitali utakaotumiwa na watu wa maeneo yote hasa walio masokoni.

Kampeni za kuwafikishia ujumbe na huduma hiyo ya kidijitali inayojulikana kama Teleza Kidijitali ilizinduliwa wiki iliyopita Dar es Salaam katika mitaa yenye shughuli nyingi hasa zinazohusu wamachinga.

Aidha, mwishoni mwa wiki NMB ilifikisha mfumo huo mpya wa Teleza Kidijitali jijini Arusha ambapo lengo kuu ni kusogeza huduma kwa wananchi ili waweze kutumia fursa mbalimbali ikiwemo mikopo nafuu.

Akizindua mfumo huo katika Soko la Kilombero jijini Arusha, Ofisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa NMB, Filbert Mponzi alisema mfumo huo ni kampeni ambayo itawafanywa Watanzania wengi kuingia katika mfumo wa kibenki.

Alibainisha kuwa kupitia mfumo huo wananchi hawatakuwa na ulazima kufika kwenye matawi ya NMB kufanya miamala yao, lakini pia watakuwa na fursa ya kupata huduma ya Mshiko Fasta ambao ni mkopo wa wateja wadogo na inayopatikana kwa njia ya NMB mkononi.

 "Kwa kupitia huduma hii, mteja atafungua akaunti na kutokana na miamala yake anaweza kujipatia mkopo wa shilingi 100,000 lakini pamoja na hilo tunawaletea NMB pesa wakala ambayo imerahisishwa zaidi," alisema.

Baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Kilombero walisema wanaishukuru benki ya NMB kwa kuwaletea huduma hiyo itakayowasaidia kupata mikopo ya fedha kwa ajili ya kujiinua kichumi.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Arusha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi