loader
Mwongozo wa kutumia makundi ya nyuki kuchavusha watolewa

Mwongozo wa kutumia makundi ya nyuki kuchavusha watolewa

SERIKALI imezindua mwongozo wa namna ya kutumia makundi ya nyuki kwenye huduma za uchavushaji wa mimea na mazao shambani.

Mwongozo huo umelenga kuwasaidia wakulima na wafugaji nyuki nchini kupata manufaa zaidi kuliko kupata asali tu.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizindua mwongozo huo, alisema utasaidia wafugaji na wakulima kumuona mdudu nyuki katika thamani yake halisi.

Pinda alisema mfugaji nyuki anaweza kuwakodisha wakulima wengine mizinga ya nyuki kwa kipindi cha msimu mmoja wa zao ambapo uzalishaji wa zao husika utaongezeka na mfugaji nyuki akilipwa ada ya uchavushaji huku pia uzalishaji wake wa mazao ya nyuki ukiongezeka maradufu.

“Ziko nchi nyingine kwa kutambua kuwa nyuki ni wachavushaji wakuu wanaotoa uhakika wa chakula wameiweka sekta hii chini ya Wizara ya Kilimo, tubadilike tukifanya vizuri kwenye ufugaji nyuki tutakuwa na uhakika wa chakula lakini pia nchi nyingi tutazishinda kwa uzalishaji asali.

“Sisi hapa tuna uwezo wa kuzalisha hadi tani 140,000 na kuendelea kwa utajiri tulionao, tatizo ni kwamba hatujafunguka licha ya serikali kuonesha dhamira ya wazi ya kutaka kukuza sekta ya ufugaji nyuki,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Ezekiel Mwakalukwa akizungumzia mwongozo huo alisema ni mkakati wa kuwasaidia wafugaji nyuki kuanzia kwenye uandaaji wa makundi ya nyuki, utunzaji wake wakiwa shambani hadi namna ya kuingia makubaliano.

Miongoni mwa vipengele ambavyo mwongozo huo unaelezea ni namna ya kuandaa makundi ya nyuki kwa ajili ya uchavushaji, usimamizi wa makundi hayo ya nyuki yakiwa shambani, utaratibu wa kuyarudisha makundi ya nyuki baada ya uchavushaji mahali unapoyatunza, usalama na huduma ya kwanza katika shamba linalopata huduma ya uchavushaji na masuala ya kuzingatia wakati wa kupanga bei ya ukodishaji makundi ya nyuki

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/521366725d86f4880d05f27b09622bfa.jpg

MKURUNGENZI wa Kampuni ya Prosperity ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mpanda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi