loader
‘Matumizi sahihi ya  ARV hupunguza vifo’

‘Matumizi sahihi ya ARV hupunguza vifo’

MKURUGENZI Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Dk Leonard Maboko amesema jamii ikizingatia mbinu mbalimbali za kinga dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), itaepusha maambukizo mapya ya virusi hivyo.

Aidha, amesema watu wanaoishi na virusi hivyo wakitumia kwa usahihi dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo (ARV), vifo vitokanavyo na ukimwi vitapungua.

Amesema katika kudhibiti janga la ukimwi katika jamii, maambukizo mapya yanapaswa kushuka na kuwa chini kuliko idadi ya vifo vitokanavyo na Ukimwi.

Dk Maboko ameihimiza jamii kuunganisha nguvu na kukomesha unyanyapaa kwa kuwa unachochea kasi ya vifo.

Alisema hayo katika mafunzo kwa wahariri na waandishi wa habari yaliyofanyika mjini hapa mwishoni mwa wiki yakiwa yameandaliwa na Tacaids kwa ushirikiano na taasisi ya Pact Tanzania.

Katika mafunzo hayo yaliyolenga kuboresha maarifa mintarafu namna ya kuripoti habari zinazohusu VVU/ Ukimwi, sambamba na uelewa wa hali ilivyo kuhusu unyanyapaa na ubaguzi, alisema vyombo vya habari havina budi kutoa mchango chanya katika jamii ili kufikia lengo la sifuri tatu ifikapo mwaka 2030 yaani kusiwepo maambukizo mapya ya VVU, kusiwepo vifo vitokanavyo na VVU/Ukimwi na kutokuwapo kabisa kwa unyanyapaa.

Kwa mujibu wa Dk Maboko, kwa kiasi kikubwa vifo ni matokeo ya watu kutokupima na kuanza dawa mapema kwa wanaobainika kuwa na maambukizo na pia kututomia dawa za kupunguza makali ya VVU ipasavyo.

“Vifo vingi ni matokeo ya watu kutokujua hali zao, kutokuanza kutumia dawa mapema na kutotumia dawa vizuri… Unyanyapaa na ubaguzi unaweza kusababisha watu wasipime na wasitumie dawa ipasavyo na matokeo yake huwa ni vifo,” alisema.

Akizungumzia unyanyapaa katika jamii kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanyika Februari hadi Aprili, 2021 katika mikoa 15 Tanzania Bara, Yahaya Mmbaga kutoka Tacaids alisema kitaifa umepungua kutoka asilimia 28 mwaka 2013 hadi asilimia 5.5 mwaka 2021.

“Kimkoa, Kilimanjaro una asilimia 19.5, huku Mkoa wa Tanga ukiwa na unyanyapaa kwa asilimia 10.5. Mkoa wa Iringa una asilimia 1.4 na Mbeya asilimia 2.8,” alisema Mmbaga.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/294826fb412aff3fa5b17e32e3568605.jpg

MKURUNGENZI wa Kampuni ya Prosperity ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Morogoro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi