loader
Mbunge ashauri vivuko vibinafsishwe kuongeza ufanisi

Mbunge ashauri vivuko vibinafsishwe kuongeza ufanisi

MBUNGE wa Kigamboni, Dk Fausitine Ndugulile (CCM) ameishauri serikali kuvibinafsisha vivuko vya Kigamboni ili kuongeza ufanisi ikiwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wameshindwa kutimizi wajibu.

Kwa mujibu wa Mbunge, MV Kazi kwa mfano, ni kivuko kipya lakini kimekuwa katika matengenezo ya mara kwa mara na hadi sasa haikifanyi kazi ingawa serikali iliahidi miezi minne iliyopita kuwa ingekifanyia matengenezo nakukirejesha majini.

Ndugulile amesema usimamizi wa vivuko umekuwa mbovu na kwamba “TEMESA wameshindwa kuvisimamia” kwa kuwa abiria kuvuka kutoka upande mmoja hadi mwingine inachukua zaidi ya dakika 45. “Vivuko hivi vitakuja kuleta maafa kama TEMESA wameshindwa kuviendesha, tuvibinafsishe kwa sekta binafsi iweze kuviongoza.”

Vilevile Ndugulile amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan akisema “Rais Samia amewafuta machozi wananchi wa Kigamboni,” lakini tozo ile inaongeza gharama katika maisha ya wananchi. Niombe huu ni mwanzo lakini tunahitaji ifutwe.”

Serikali ilitangaza juma lililopita kupunguza tozo katika daraja la Kigamboni “Nyerere Bridge” kwa karibu asilimia 50 ili kuweka unafuu wa maisha kwa wananchi wakazi wa Kigamboni.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/0384ef2db16360b3de54711517fe0cc6.jpg

WIZARA ya Afya inaendelea na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi