loader
Mbunge akataa majibu ya Naibu Waziri

Mbunge akataa majibu ya Naibu Waziri

Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu amekataa majibu ya Naibu Waziri Tamisemi, John Silinde na kuliambia bunge kuwa majibu hayo ni ya uongo.

Kanyasu aliyasema hayo kufuatia majibu ya Naibu Waziri huyo wa Tamisemi kuhusu Mji wa Geita kuwa Manispaa kufuatia taratibu zote kukamilika na hivyo kufikia viwango vya kupewa hadhi ya manispaa.

Akijibu swali kwa niaba ya Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Silinde amesema wizara ilipokea mapendekezo ya kupandisha hadhi halmashauri ya Mji Geita kuwa Manispaa na baada ya kufanyiwa uhakiki na timu ya wataalam kutoka wizarani, kati ya vigezo 21 Halmashauri ya Mji wa Geita ilikuwa imekidhi vigezo 18 sawa na asilimia 85.

Aliongeza kuwa halmashauri haikuweza kupandishwa hadhi kwa kuwa ililazimu kukidhi vigezo vyote kwa pamoja kwa mujibu wa muongozo wa kuanzisha maeneo ya utawala wa mwaka 2014, ili kupandishwa hadhi ya kuwa Halmashauri ya Manispaa.

foto
Mwandishi: Adam Lutta, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi