TARARIBU za ununuzi kwa ajili ya ujenzi wa Daraja katika Mto Pangani litakalounganisha Vijiji vya Bweni na Pangani lenye urefu wa meta 525, ziko hatua za mwisho kwa ajili ya kusaini mkataba.
Hayo yamesemwa bungeni leo na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mwantumu Mzamilu Zodo, aliyehoji kuhusu ujenzi wa Daraja la Bweni Wilaya ya Pangani.