loader
TANESCO yaja kisasa zaidi  Mwanza

TANESCO yaja kisasa zaidi Mwanza

ZAIDI ya wateja 170,000 wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) Mkoa wa Mwanza, wanatarajia kunufaika na huduma ya Ni-konnekt app kutoka shirika hilo.

Hayo yamesemwa leo Mei 24, 2022 na Ofisa Uhusiano Huduma kwa wateja kutoka shirika hilo kwa mkoa wa Mwanza, Flaviana Moshi, wakati wa kikao kazi na wakandarasi kutoka mkoani Mwanza.

‘’TANESCO imeendelea na uboreshaji wa huduma zetu mbalimbali, ikiwemo huduma ya Ni-konnekt app inayopatikana kwa simu janja na simu za kawaida,’’ amesema Moshi.

Amesema huduma hiyo kupitia Web Portal kwa simu za Android inapatikana kupitia ‘google play store’, simu za iphone inapatikana kupitia mfumo wa IOS.

Naye Ofisa Mifumo ya Biashara wa TANESCO Mkoa wa Mwanza, Raymond Matovu amesema mfumo wa Ni-konnekt app, utawasaidia wateja wao kupata huduma za kuomba umeme.

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi