loader
Tatu Mzuka 14 wadakwa Arusha

Tatu Mzuka 14 wadakwa Arusha

VIJANA 14 wanaodaiwa kuwa miongoni mwa wanaoendesha vitendo vya uporaji mkoani Arusha wakitumia pikipiki, wanaojulikana kama Tatu Mzuka wamekamatwa na Jeshi la Polisi wakiwa na pikipiki zao 12.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema waliendesha operesheni maalum ya kuwakamata wahalifu hao kuanzia Mei 19, mwaka huu, huku baadhi ya pikipiki zikiwa hazina namba za usajili rasmi na nyingine ikiandikwa RIP Scober.

Amesema watumiwa hao wamehojiwa kwa kina na kukiri kufanya matukio ya uporaji na kwamba wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine waliotajwa na wenzao.

foto
Mwandishi:  Apollo Kiity

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi