loader
Serikali  yatangaza neema kwa wastaafu

Serikali yatangaza neema kwa wastaafu

KATIBU  Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Profesa Jamal Katundu ametangaza kiwango kipya cha kikokotoo cha mafao ya mkupuo ambapo sasa ni asilimia 33 kwa mifuko yote ya hifadhi ya jamii.

Akizungumza leo Mei 26, 2022 Profesa Katundu amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya makubaliano kati ya Serikali, Chama cha Waajiri Nchini (ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) bada ya kusitishwa kwa kanuni zilizotengenezwa Desemba 28 mwaka 2018.

“Kanuni  mpya ya kikokotoo ambayo tunaitangaza  leo inaongeza kiwango cha mkupuo kutoka asilimia 25 iliyokataliwa mwaka 2018 hadi asilimia 33 kwa zaidi ya wanachama milioni 1.3 sawa na asilimia 81 ya wananchama wote wa mifuko ambao ni milioni 1.69.

Amesema kikokotoo hchoi pia kinaongeza pensheni ya mwezi kutoka asilimia 50 ya sasa hadi asilimia 66 kwa waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF ambao ni asilimia 19 ya wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

Amesema mifuko ya pensheni ya NSSF na PSSSF itaimarika na kuwa endelevu na hivyo kuwa na uwezo wa kuongeza pensheni ya kila mwezi kwa kuzingatia tathmini zitakazo fanyika kila baada ya miezi mitatu

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4c311a442aa43f753d465b79e5ae89ff.jpg

MKURUNGENZI wa Kampuni ya Prosperity ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi