loader
Sekta binafsi inahusika vipi Mwaka wa Lishe Afrika?

Sekta binafsi inahusika vipi Mwaka wa Lishe Afrika?

MWAKA 2022 ni mwaka wa lishe Afrika, hiyo ndiyo kaulimbiu ya Umoja wa Afrika kwenye Siku ya Afrika mwaka huu.

Kila mwaka Mei 25 ni maadhimisho ya Siku ya Afrika duniani. Siku hii ni malaum kwa ajili ya kutafakari maendeleo ya bara la Afrika na changamoto zinazokabili nchi zake. Ingawa kumekuwa na mafanikio mengi tangu Afrika ipate uhuru kutoka kwa wakoloni, lishe bado ni tatizo kubwa barani Afrika.

Mwaka huu lishe ndio ajenda kuu pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama ya kunywa.

"Upatikanaji wa maji safi na salama ni sehemu kuu ya kuboresha lishe kwa Afrika," anasema Biram Fall, Meneja Mkuu wa QNET Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

 

Akizungumza kupitia taarifa kwa vyombo vya habari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika, Fall anasema, kampuni hiyo inaungana na jitihada za serikali kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama Tanzania.

“Sisi tulishiriki katika Siku ya Maji Duniani ya mwaka huu, huko Dakar, Senegal ambapo tulionesha vifaa kadhaa vya kusafisha maji kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya uchujaji wa wa maji majumbani inayoitwa HomePure,” aliendelea kusema.

Teknolojia hii ya kuchuja maji majumbani ni mchango muhimu katika jitihada za kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kama sehemu ya kuboresha lishe na afya.

Kwa mujibu wa ripoti ya Maendeleo ya Upatikanaji wa Maji duniani iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa; "Katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, ni asilimia 24 tu ya wakazi wanapata maji safi ya kunywa.”

"Kama takwimu zinavyoonesha, kuna haja ya mashirika ya umma na ya kibinafsi kuongeza juhudi za kuziba pengo la upatikanaji wa maji safi na salama Afrika," Fall aliendelea kusema.

“Kwetu sisi, suala la upatikanaji wa maji safi na salama ni kipengere muhimu cha maendeleo kwa Afrika na ni sehemu kuu ya mkakati wetu wa kimataifa kuleta suluhisho endelevu ya upatikanaji wa maji salama ya kunywa,” aliongezea.

Kati ya juhudi za QNET kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama Afrika ni pamoja na ushirikiano wa kampuni hio na shirika la Ecomatch katika kulinda vyanzo vya maji nchini barani Afrika.

Kupitia kampeni inayoitwa Green Initiative kampuni hio imepanda miti zaidi ya 1000 katika mabara kadhaa ikiwemo Afrika Mashariki.

Kupitia mradi huu, QNET imepanda miti Kenya na nchini Tanzania, QNET imesaidia jamii mbalimbali kuchimba visima ili kuongeza upatikanaji wa maji safi. 

Kwa mfano Mkoa wa Iringa, kampuni hiyo imesaidia uchimbaji wa visima takribani 45 pamoja na upandaji wa miti ya matunda.

Kupitia mradi huu, wakazi wa Iringa wanapata ajira na umiliki wa mashamba na kutumia maji ya visima kueneza kilimo cha umwagiliaji hivo kuongeza upatikanaji wa lishe bora.

Kwa mujibu wa shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), uboreshaji wa mbinu za kilimo na kulinda vyanzo vya maji husaidia kuhakikisha ubora wa maji kwenye maeneo yanayo tegemea  maji hayo.

"Ajenda ya Afrika ya 2030 na hatua za kuleta mabadiliko katika usambazaji wa maji safi na Ajenda ya Afrika 2063 ya maendeleo, zote zinazingatia uboreshaji wa lishe kama msingi wa maendeleo endelevu kwa bara la Afrika, hivo ni wajibu wetu na sekta binafsi kwa ujumla kuongeza kunguvu na kushirikiana na serekali  kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama," anasema.

Hivi sasa, zaidi ya watu bilioni 2.2 barani Afrika wanakosa maji safi na salama na hii ndiyo sababu Bunge la Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika limeweka ajenda kuu ya siku ya Afrika mwaka huu kuwa Lishe na Upatikanaji wa maji safi na salama.

Rasilimali kubwa ya Afrika ni watu wake, kwa hivyo, kuleta maendeleo chanya katika bara hili, ni muhimu kuongeza upatikanaji wa lishe na maji salama kwa watu wake. Umoja wa Afrika unasisitiza umuhimu wa upatikanaji wa lishe bora hususan kwa wanawake, vijana na watoto.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/357808e83a2f09855406eb9e6a339cdd.jpg

HAPA nchini Agosti 23 mwaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi