loader
Serikali yapiga marufuku ‘kibao kata’, ‘Vigoma’

Serikali yapiga marufuku ‘kibao kata’, ‘Vigoma’

SERIKALI imepiga marufuku vitendo vya wananchi kucheza ngoma zijulikanazo kama vigoma na kibao kata nyakati za usiku bila staha ikisema ni kinyume cha maadili na sheria za nchi kwa kuwa huchochea uasherati, udhalilishaji wa utu na heshima ya mwanamke.

Naibu Waziri ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini, amesema Jijini Dar es Salaam: “Ngoma hizo huchochea kueneza magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya kujamiana na mimba zisizotarajiwa lakini pia ni ukatili dhidi ya watoto wanaotumikishwa kucheza ngoma hizo."

"Uchunguzi uliofanywa na vyombo vya dola umebaini kuibuka kwa baadhi ya wanawake wanaofundisha vitendo na kufanya matendo ya ngono kwa kutumia vifaa hatarishi kama chupa za bia, soda, mahindi ya kuchoma, ndizi na matango."

"Baadhi yao wameunda makundi ya whatsup ilikuweka picha zao za utupu na wengine huziweka katika mitandao tofauti tofauti ya kijamii, uchunguzi zaidi umebaini kuwa wanawake na mabinti wanaonekana kukubuhu kufanya vitendo hivyo husafirishwa na kwenda Ughaibuni na kutumikishwa katika biashara ya ukahaba, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi" amesema Sagini

Ameongeza kuwa Wizara kwa kushirikiana na vyombo vya Dola imewakamata mabinti 16 wanaojihusisha na vitendo hivyo kutoka maeneo tofauti tofauti Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Mwanaidi Khamis amesema wananchi wanatakiwa wawewawazi katika kuibua vitendo viovu.

"Serikali ni watu na watu ndio sisi kunapokuwa na tatizo unatakiwa kumfata kiongozi wa kijiji kumpa taarifa katika kupambana na ukatili."

Kwa upande wake  Kamanda wa Kanda Maalumu, Jumanne Mulilo, amesema kuwa  jeshi la Polisi tumejipanga kikamilifu katika kupinga vitendo viovu vya uvunjivu wa sheria.
 

foto
Mwandishi: Na Brighiter Masaki

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi