loader
Yanga yaachana na Ntibazonkiza

Yanga yaachana na Ntibazonkiza

KLABU ya Yanga imeachana na kiungo mchezeshaji wa timu hiyo, Saido Ntibazonkiza, baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili.

Wiki iliyopita mchezaji huyo aliondolewa kwenye kikosi cha timu hiyo na mwenzake Dickson Ambundo, baada ya wawili hao kubainika kutoroka kambini jijini Mwanza wakati timu hiyo ikijiandaa kwa pambano la nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Simba, ambalo walishinda 1-0.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka klab ya Yanga, mkataba wa miaka miwili wa Ntibazonkiza umefikia kikomo jana, Mei 30 na kuna taarifa kwamba tayari uongozi wa timu hiyo ulishaanza mazungumzo ya kumwongezea mkataba mpya, lakini aligoma kufanya hivyo.

Inaelezwa kuwa mara baada ya Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi kumwondoa kambini mchezaji huyo pamoja na mwenzake Ambundo na kutakiwa wakutane wiki hii Dar es Salaam, inaarifiwa kuwa Ntibazonkiza alirejea Dar es Salaam na kubeba kila kilicho chake na kurudi kwao Burundi.

Uongozi wa Yanga umemshukuru Ntibazonkiza kwa kipindi chote alichokuwa nao na wanamtakia kila la kheri na mafanikio katika maisha yake ya soka nje ya klabu hiyo.

foto
Mwandishi: Mwandishi wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi