loader
JKT yawaita kambini wahitimu kidato cha sita

JKT yawaita kambini wahitimu kidato cha sita

JESHI la kujenga Taifa (JKT) limewaita vijana waliohitimu kidato cha sita kwa mwaka 2022 kujiandikisha kushiriki mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria yanayo tarajiwa kuanza  Juni 03 hadi 17 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mei 31, 2022, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa, Brigedia Jeneral Hassan Mabena amesema JKT tayari imeshaandaa kambi kwa ajili ya kupokea na kufundisha wanafunzi hao.

Kambi zilizo tayari ni pamoja na JKT Rwamkoma (Mara), JKT Msange (Tabora), JKT Ruvu (Pwani) na JKT Mpwapwa, JKT Makutuppra (Dodoma). Zingine ni JKT Mafinga (Iringa), JKT Mlale (Ruvuma), JKT Mgambo na JKT Maramba (Tanga), JKT Mkuyuni (Arusha) na JKT Bulombora, JKT Kanebwa na JKT Milundikwa (Rukwa).

Pia kuna JKT Mtabila (Kigoma), JKT Itaka (Songwe), JKT Luwa  na JKT Milundikwa (Ruvuma), JKT Nachingwea (Lindi) JKT Kibiti (Pwani) na JKT Oljoro (Arusha).

Amesema Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoa Pwani ambapo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

"JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa, Bukta ya ranging ya Dark Blue yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, mrefu unaoishia magotini isiyo na zipu, tisheti ya rangi ya kijani, raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue"

"Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari, soski ndefu za ranging nyeusi, nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi, tracki suti yenye rangi ya kijani au bluu na nyaraka zote zinazohitajika katika udahili wa kujiunga na elimu ya juu zikiwemo cheti cha kuzaliwa, vyeti vya kuhitimu kidato cha nne pamoja na nauli ya kwenda na kurudi," amesema

foto
Mwandishi: Brighiter Masaki

2 Comments

 • avatar
  Lazaro n. Liki
  01/06/2022

  Mimi nimemaliza form six katika chuo cha ualimu butimba sijaona jina langu kwenye selection za jkt.. naomba kupangiwa maana ninahitaji kulijenga taifa

 • avatar
  clara Mambia
  17/06/2022

  kuna vijana zaidi ya watano akiwemo wangu, walianza safari ya kuelekea Luwa JKT, Rukwa wamekwama baada ya basi walilokuwa wamepanda kupata shida Iringa , ambapo ilibidi kuanza safari asubuhi baada ya kufaulishwa kwenye gari nyingine mpaka wakati huu bado wako safarini, kwa changamoto hii sijui watafika saa ngapi. Naomba taarifa hii ifike mahali husika ili kutambua kuwa vijana wako safarini

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi