loader
TBL wazindua bia mpya

TBL wazindua bia mpya

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) Mkoani Mwanza imezindua Bia mpya mbili ambazo zina ladha nzuri na zenye urahisi wa ubebaji wake.

Meneja Mauzo wa TBL Mkoani Mwanza Yuda Ryaga amesema Leo Jijini Mwanza kuwa bia hizo mpya zilizoingia sokoni ni Flying Fish na Kilimanjaro Litre.

Alisema vinywaji hivyo vinavyoingia sokoni vimetengenezwa kwa ubora wa hali juu kutokana na mazao yanayolimwa hapa nchini zikiwa na kilevi cha asilimia 4.5.

Bia hizo mtu anaweza kununua na kupeleka kokote kule kwani hazihaji kurudisha chupa.

"Tunauza shilingi 40,000 chupa 24 ambapo kwa rejareja mteja unanunua kwa 2000/= kwa chupa"

Ryaga amewataka wakulima wa shayiri na ngano hapq nchini kuongeza uzalishaji wa mazao hayo kwani kuna uhakika wa soko la mazao hayo.

foto
Mwandishi: Suleiman Shagata,Mwanza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi