loader
CRDB yajipanga kunufaisha wateja kupitia ‘Mzigo Flex’

CRDB yajipanga kunufaisha wateja kupitia ‘Mzigo Flex’

Katika juhudi za kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na riba ya asilimia tisa (9%) baada ya kujiwekea akiba, Benki ya CRDB imejipanga kuendelea kuhamasisha wananchi kupitia promosheni ya Mzigo Flexi inayoendeshwa maeneo maeneo mbalimbali Dar es salaam

 Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika viunga vya Tawi la CRDB Benki lililopo Mtaa wa  Azikiwe jijini Dar es salam Mapema leo, Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili amesema: “Sisi kama Benki tumeamua kuwafikia Watanzania na kuwapa elimu ya fedha ili kuwajengea utamaduni wa kujiwekea akiba kwa malengo ya muda mfupi, kati na mrefu”.

 

"Sambamba na kuwapa elimu lakini pia kupitia mpango huu Benki inatoa riba ya hadi asilimia 9 ili kutoa hamasa ya kuweka akiba ambapo kupitia promosheni ya Mzigo Flexi, mteja anaweza kuweka amana kwa muda wa kati ya miezi 3, 6, 12 au 24,” alisema Adili.

Promosheni ya ‘Mzigo Flexi’ inalenga watu binafsi, vikundi, taasisi na wafanyabiashara na mteja anaweza kuwa na mpango wa akiba wa ‘Mzigo Flexi’ zaidi ya mmoja na kuwekeza kwenye mikataba mingi.

Ameeleza kuwa mkataba utakuwa huru na bidhaa haina ada yoyote na riba inalipwa kwa akaunti ya kibinafsi ya mteja kulingana na kipindi cha riba kilichokubaliwa ambacho ni kila mwenzi, robo mwaka, nusu mwaka, kila mwaka au wakati wa kukomaa.

 Iwapo mteja ataamua kughairi utaratibu wa ‘Mzigo Flexi’, atalazimika kupoteza asilimia 50 ya riba aliyopata na kuendelea kuweka fedha chini ya utaratibu mwingine wa kawaida wa benki.

 Kupitia huduma hiyo, wateja wanaweza kupata mpango wa akiba wa “Mzigo Flexi” huo kupitia tawi lolote la Benki ya CRDB nchi nzima lakini pia anaweza kupata fomu ya maombi kupitia tovuti ya Benki na kuwasilisha katika tawi lolote la Benki ya CRDB baada ya kuzijaza.

 

 

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi