Benki ya ACB imekutana na wateja wake jijini Mwanza, ikiwa ni sehemu ya programu yake ya kudumisha uhusiano kati yake na wadau hao.
Katika tukio hilo lililofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel alikuwa mgeni rasmi.
Mkutano huo uliokutanisha wadau hao uliitoshwa na Mkurugenzi wa Akiba Commercial Bank (ACB), Silvest Arumasi na pande zote zilibadilishana mawazo ya namna bora ya kuboresha huduma ya kifedha kwa manufaa ya pande zote mbili.
Meneja wa ACB tawi la Mwanza, Herieth Bujiku alipata wasaa wa kuzungumza na wateja wa benki hiyo yenye matawi katika sehemu mbalimbali hapa nchini.
Kabla ya kuanza kwa tukio hilo, wafanyakazi wa ACB ndio waliokuwa mstari wa mbele kuwakaribisha wateja waliohudhuria tukio hilo.