loader
Wasanii wa singeli kunogesha ZIFF

Wasanii wa singeli kunogesha ZIFF

WASANII wa muziki wa singeli wanatarajiwa kupamba Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) litakalofanyika kuanzia Juni 18-26 mwaka huu.

Tamasha hilo linatarajiwa kushirikisha filamu zaidi ya 100 na linatarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake.

Akizungumza na HabariLeo, Mratibu wa tamasha hilo, Martin Mhando, amesema tamash hilo litapambwa na wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Aliwataja baadhi ya wasanii wa singeli walioalikwa kuwa ni Meja Kunta, Dullah Makabila na Mzee wa Bwax.

Akizungumzia hilo, Meja Kunta, amesema amejiskia furaha kushiriki kwenye tamasha hilo, ikiwa ni mara yake ya kwanza.

foto
Mwandishi: Brighiter Masaki

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi