loader
PeakTime waja kiburudani zaidi

PeakTime waja kiburudani zaidi

KAMPUNI inayoshughulika na kusimamia michezo na burudani, PeakTime imetambulisha rasmi Lebo na  msanii chipukizi wa singeli, Mwajuma Othman 'Mwajuma Chaupepo'.

Pia msanii huyo ametambulisha EP yake mpya itakayozinduliwa Jumamosi wiki hii ukumbi wa Small Planet Tabata,  Dar es Salaam.

Akizungumzia ujio wa msanii huyo, Mratibu wa Matukio wa kampuni hiyo, Bakari Khatibu, amesema wameamua kuleta ushindani wa wasanii wa kike katika muziki huo.

"Yote ni kuleta mabadiliko katika tasnia ya muziki na ushindani kiujumla, itasaidia kuleta hamasa kutokana na wasanii wa kike kuwa wachache, " amesema.

Amesema licha ya  Peaktime kushughulika na mchezo wa masumbwi, hivi sasa wanaleta burudani nyingine ya tofauti kwa mashabiki na wadau wote wa michezo, kwani hata mchezo wa masumbwi umekua ukichagizwa sana na mziki wa singeli, " amesema Bakari Khatibu.

Kwa upande wake Mwajuma Chaupepo, amesema hadi sasa hajaona msanii mwanamke anayeweza kumpa changamoto kwa upande huo.

"EP hiyo yangu ina nyimbo saba, ambazo ni Ndoa, Ndala, Hatufanani, Fresh,  Singeli Tamu, Tatizo Noti, Vibe na Baby,” amesema.

foto
Mwandishi: Brighiter Masaki

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi