loader
Biashara Tanzania, China yafikia dola bilioni 6.7

Biashara Tanzania, China yafikia dola bilioni 6.7

KIWANGO cha biashara kati ya Tanzania na China kimezidi kukua na kufi kia Dola za Marekani bilioni 6.7. Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mambo ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wu Peng alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari vya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

Alisema Tanzania inatarajia kufungua ubalozi mwingine nchini humo katika mji wa Shanghai na kwamba nchi hizo zinaendelea kujadiliana ili nchi hiyo inunue mazao ya bahari katika kukuza uchumi wa buluu. Alisema licha ya athari za janga la Covid-19, biashara baina ya nchi hizo imezidi kuimarika.

Peng alisema mwaka 2020 biashara ilikuwa kwa asilimia 9.5 na mwaka 2021 kukua kwa asilimia 6.74. Alisema Tanzania inatarajia kuwa na balozi tatu nchini China ili kukuza uhusiano zaidi hasa mwingiliano wa watu katika miji ya Beijing, Guangzhou na hivi karibuni inatarajia kufungua ubalozi Shanghai.

Akizungumzia Tanzania kunufaika na fedha ambazo mwaka jana Rais Xi Jinping wa China aliahidi kuipatia Afrika zaidi ya Dola za Marekani bilioni 40, Peng alisema Tanzania ni moja ya nchi zilizopewa kipaumbele kwa kuingiza bidhaa kutoka nchini humo.

“China ni watumiaji wazuri wa bidhaa za soya na miaka yote tumekuwa tukiingiza kwa wingi kutoka nchini Marekani, lakini baada ya kuingia katika migogoro ya kiuchumi na nchi hiyo sasa tumeanza kuingiza bidhaa hii kutoka Tanzania,” alisema

foto
Mwandishi: Na Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi