loader
Jeshi la EAC kuingia DRC kutuliza ghasia

Jeshi la EAC kuingia DRC kutuliza ghasia

WAKUU wa nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki wameagiza jeshi la Kikanda kushirikiana na jeshi na vikosi vya ulinzi na utawala vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kuleta utulivu na kulinda amani nchini humo.

Wakuu hao wa Jumuiya wamekutana nchini Kenya na kukubaliana kuwa wapiganaji katika sehemu ya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wasitishe mapigano mara moja na kukomesha uhasama ili shughuli za kijamii, kitamaduni na uchumi ziweze kurejea.

Katika kikao hicho kilicho tanguliwa na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kutoa mataifa yote saba wanachama kiliadhimia kuwa wapiganaji hao pia wajiondoe katika maeneo waliyoyachukua ili kuruhusu raia wa DRC kujisikia salama.

Katika taarifa iliyotolewa na Jumuiya hiyo, Viongozi hao wamekubaliana kuendelea na upatanisho na kutafuta haraka suluhu ya kudumu ya amani katika mzozo huo hasa maeneo ya Kaskazini na Kusini mwa jimbo la Kivu na Ituri.

 

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi