loader
Watatu kortini kwa kuua mtoto chekechea

Watatu kortini kwa kuua mtoto chekechea

JESHI la Polisi mkoani Geita limewafikisha mahakamani watu watatu kutoka wilayani Nyang’hwale mkoani Geita kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa chekechea mwenye umri wa miaka saba (jina tunalihifadhi).

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Kamishina Msaidizi (ACP), Henry Mwaibambe ametoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari mjini Geita ikiwa ni siku chache tangu kutokea kwa mauaji hayo Juni 12 mwaka huu.

Amewataja watuhumiwa hao ni Sita Bujiku Msabila (52), ambaye ni mganga wa tiba asilia pamoja na Mathias Shilole (26) na Lucy Ndelema (75) ambao ni wakulima, wote ni wakazi wa kijiji cha Kilimani, Kata ya Ibambila wilayani Nyang’hwale.

“Siku ya Juni 12 mwaka huu majira ya mchana, Dorcus akiwa na mwenzake aitwaye Malemi Musa Adrian (miaka mitano), wanachunga mbuzi na dama alinyakuliwa na watuhumiwa Sita Bujiku Msabila na mwenzie Mathias Shilole.

“Kisha walimficha sehemu isiyojulikana na baadaye kumbaka, kumlawiti na kumvunja shingo yake baada ya kumuua waliuficha mwili wa marehemu kwenye shimo dogo lenye kina cha futi tatu.

“Mwili wa marehemu baada ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari ulibainika kuwa umebakwa na kulawitiwa na kisha kunyongwa,” amesema Kamanda Mwaibambe.

Kamanda Mwaibambe amesema uchunguzi wa tukio hilo umebaini ukatili huo unahusishwa na imani za kishirikina pamoja na ramli chonganishi, ambapo jeshi la polisi limejiridhisha watuhumiwa hao walihusika moja kwa moja.

“Tumepewa maagizo na Mkuu wa Mkoa namna ya kukomesha matukio haya, hatuwezi kusema tutatumia mbinu, gani lakini siku zote serikali ina mkono mrefu na tuna imani hawa wanaojihusisha na vitendo kama hivo tutawafikia, tutawakamata na sheria itachukua mkondo wake,” amesema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/cf9c45b7a890eb636268e01324148399.jpg

MKURUNGENZI wa Kampuni ya Prosperity ...

foto
Mwandishi: Yohana Shida, Geita

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi