loader
Mkurugenzi Arusha, wenzake wasomewa mashtaka mapya sita

Mkurugenzi Arusha, wenzake wasomewa mashtaka mapya sita

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dk. John Pima (44) na wenzake wawili wamepandishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa mashtaka sita likiwemo la utakatishaji fedha na ubadhirifu wa kiasi cha Sh milioni 103 wakati wakiwa waajiriwa Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Dk Pima tayari akiwa na wenzake wanne, walifunguliwa mashtaka manne likiwemo la uhujumu uchumi katika mahakama hiyo wiki iliyopita. Walioshitakiwa alikuwa ni Mariamu Mshana (43), mweka hazina wa Jiji, Innocent Maduhu (40) Mchumi, Nuru Saqware Mchumi na Alex Tihema. 

Watuhumiwa hao wanadaiwa kumdanganya mwajiri na kujipatia kiasi cha Sh milioni 67 wakati wakijua wazi kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Arusha, Richard Jacopiyo alidai Juni 21, kuwa Dk. Pima mkazi wa Lemara Jijini Arusha, Mariamu Mshana, na Innocent Maduhu wote kwa pamoja wanadaiwa Machi 23 na 25 mwaka huu waliweza kumdanganya mwajiri na kufanikiwa kuchota kiasi cha Sh milioni 103 na kutumia kwa mambo yao binafsi.

Jacopiyo alisema mbele ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Batony Mwakisu kuwa shitaka la pili ni washitakiwa wote kwa pamoja Machi 27 mwaka huu wakiwa waajiriwa wa Jiji la Arusha walitumia nyaraka za uongo zenye lengo la kumdanganya mwajiri kwa kutumia jina la Maduhu na kuandika dokezo la kujipatia Sh milioni 103 kwa ajili ya kununua mchanga, moramu kwa ajili ya kutengeneza matofali wakati wakijua wazi kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Shitaka jingine, ni kumdanganya mwajiri na kufanikiwa kuomba fedha za safari kiasi cha Sh milioni 103 na ujenzi wa kiwanda cha matofali kwa kutumia jina la mshitakiwa wa tatu. 

Mwendesha mashtaka alisoma shitaka la nne kuwa watuhumiwa wote kwa pamoja walimdanganya mwajiri kwa kutumia nyaraka ya uongo kuwa mshitakiwa wa tatu amefanya marejesho ya safari na kufanikiwa kuchotaka kiasi cha Sh milioni 103 wakati wakijua wazi kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Shitaka la tano ni la utakatishaji fedha haramu kwani ilidaiwa kuwa Aprili 1 mwaka huu mshitakiwa huyo alifanikiwa kununuwa gari lenye namba za usajili T844DYY Subaru Forester wakati akijua wazi kuwa fedha hizo ni zao la ubadhilifu na ufujaji wa cha Sh milioni 103 zilizoibwa Jiji la Arusha.

Mwendesha mashitaka huyo wa Takukuru akisaidiwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Janeth Segule alisema shitaka la sita ni kujipatia kiasi cha Sh milioni 103 na kuzifanyia manunuzi mbalimbali wakati wakijua wazi kuwa zao la fedha hizo ni la uhalifu.
 
Washitakiwa wote wamekana mashitaka hayo sita na Mwendesha Mashitaka wa Takukuru amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kesi hiyo iliyoahirishwa hadi Julai 5 mwaka huu.

Watuhumiwa wote bado wako rumande na dhamana yao iko wazi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/834b9df26da6cd835116218da2ed5b89.jpg

WIZARA ya Afya inaendelea na ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi