loader
RC Katavi atoa maagizo mradi wa maji Kibaoni

RC Katavi atoa maagizo mradi wa maji Kibaoni

MKUU wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, amemtaka mkandarasi M/s Jemason Investment Co. Ltd, anaetekeleza mradi wa maji Kibaoni halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele, kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana, ili ifikapo Juni 30 kazi hiyo inakamilika.

Mrindoko ameyasema hayo alipotembelea mradi huo wa maji Kibaoni kwenda vitongoji vya Ndemanilwa, Kakuni, Ushirika na Isamvu,  unaotekelezwa kwa fedha za UVIKO-19, ambapo amesema mkandarasi huyo ahakikishe hadi kufikia Julai mosi mwaka huu vituo vyote vinatoa maji.

"Hayo ndio maelekezo ya Mheshmiwa Rais,  ni lazima yazingatiwe wala hakuna wa kuyabadilisha au kuyarekebisha, ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi, lakini pia ni moja kati ya hatua za kuhakikisha wamama na wababa wanatuliwa ndoo kichwani kwa maana ya kupata maji katika umbali mdogo sana," alisema Mrindoko.

Awali akitoa taarifa kwa mkuu wa Mkoa, Meneja RUWASA Wilaya ya Mlele, Mhandisi Gilbert Isaac amesema changamoto kubwa iliyojitokeza ni mkandarasi kuchelewa kufika eneo la ujenzi kwa maana ya kuanza ujenzi, pia kasi yake ya kuendelea na utekelezaji wa majukumu yake kuwa ndogo kulinganisha na muda wa mkataba.

Amesema gharama za mradi huo ni Sh milioni 706, ikiwa ni gharama za ujenzi wa tenki la maji lenye ukubwa wa lita 300,000 juu ya mnara wa mita 12, uchimbaji wa mitaro urefu wa Km 11.2, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 11 kwa kijiji cha Kibaoni na kazi za uchimbaji wa mitalo.

"Mradi huu wa upanuzi ni mradi unaotumia kisima kirefu kilichochimbwa mwaka 2011 chenye uwezo wa kuzalisha lita 22,000 kwa saa, ambapo awali tulikuwa tunatumia matanki mawili madogo yenye ujazo wa lita 90,000, hivyo kufanya wananchi kutokuwa na maji ya kutosha,"alisema Mhandisi Isaac.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9713b1c0dd1aa8255503d9db2aaee62c.jpg

WIZARA ya Afya inaendelea na ...

foto
Mwandishi: Swaum Katambo, katavi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi