loader
Auawa kwa debe mbili za mahindi

Auawa kwa debe mbili za mahindi

POLISI Mkoa wa Katavi inawashikilia watu watano kwa tuhuma za kudaiwa kumuua Hamisi Hassan mkazi wa Kijiji cha Kambuzi mkoani humo, kwa kumpiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake wakimtuhumu kuiba debe mbili za mahindi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Hamad Makame, amesema watuhumiwa baada ya kumuua waliufukia mwili wake kwenye shimo.

Kamanda Makame amesema watuhumiwa hao walimkamata Hamisi Hassan, baada ya kuiba mahindi hayo na kumpeleka ofisi za kata kisha viongozi wa kijiji kuwaamuru watuhumiwa kumpeleka kituo cha polisi.

Ameongeza kuwa watuhumiwa hao walikaidi kufanya kama walivyoelekezwa, ndipo walipochukua uamuzi wa kutokomea naye kusikojulikana na kutekeleza unyama huo na baada ya kufanya kitendo hicho mwili wake waliufukia kwenye shimo.

"Jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa ya kupotea kwa marehemu Hamis, walianza msako mara moja na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa mkoani Tabora, kisha kuwarudisha Katavi kwa ajili ya kuendelea na taratibu zingine za kisheria,"alisema ACP Makame na kuongeza kuwa:

"Watuhumiwa waliliongoza Jeshi la Polisi kuelekea katika eneo walilofukia mwili huo baada ya kumuua na kufanikiwa kuupata ukiwa umeharibika, kisha kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi."

Kamanda Makame aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Joseph John (32), Pasichal Andrew (37), Emmanuel Malela, Didas Mrisho, huku akisema wanaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo.

Amesema baada ya upelelezi kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili na kuwataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/7a50f490f4ec94a79cf05f4a0f081579.jpg

WIZARA ya Afya inaendelea na ...

foto
Mwandishi: Swaum Katambo, katavi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi