loader
‘Wizara iwe kitovu cha fursa sekta ya mawasiliano’

‘Wizara iwe kitovu cha fursa sekta ya mawasiliano’

WIZARA ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, inakusudia kuwa kitovu cha fursa katika Sekta ya TEHAMA kitaifa na kimataifa.

Hayo yamesemwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Jim Yonazi, wakati akifungua kikao Kazi cha uchambuzi wa fursa za kiuchumi za sekta ya mawasiliano kitaifa na kimataifa jijini Dodoma leo.

Dk. Yonazi amesema kuwa  kusudi la kikao kazi hicho ni kuangazia fursa za kisekta zilizopo nchini na mchango wake katika kukuza uchumi wa nchi.

 Pia ameongeza kuwa serikali imelenga kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya habari, mawasiliano na TEHAMA, ili waweze kutumia vyema fursa zinazokuwa zinajitokeza ndani na nje ya Tanzania. 

“Serikali imeweza kuweka mikakati ya kuwajengea uwezo watu pamoja na wadau, ili kuhakikisha tunakuza sekta hii ya mawasiliano, kama mnavyofahamu lazima tutekeleze mpango wa maendeleo kwa kuangalia yaliyomo ndani ya nchi yetu pamoja na mambo yanayoweza kuhamasisha,”alisema. 

Amesema wizara hiyo ina jukumu la kuchambua na kuangalia ni nchi zipi Tanzania inaweza kushirikiana nazo, lakini pia kuangazia suala la ujenzi wa minara na kuongeza uwezo wa kutumia simu janja pamoja na usalama wa mtandao.

“Tunatakiwa kuwa wizara ya mfano kwa kupanua wigo wa fursa za kiuchumi na kuandika historia kwa kuifanya sekta ya mawasiliano kuchangia kwa kiwango kikubwa mabadiliko na mageuzi katika uchumi wa nchi yetu," amesema Dk. Yonazi.

Ameongeza kuwa lengo kubwa la kikao hicho ni kuiwezesha Tanzania kufikia malengo ya kukuza uchumi kupitia TEHAMA sambamba na fursa zingine zilizo kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA wa Wizara hiyo, Mulembwa Munaku, amesema kuwa amepokea maagizo aliyoyatoa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, wataenda kujadili kwa kina na kuona mkakati watakaokuja nao, ambao utasaidia TEHAMA kuchangia pato la taifa kwa asilimia 3 ifikapo 2025.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d1b7bfca4db78121cce508aeea640ef5.jpg

MKURUNGENZI wa Kampuni ya Prosperity ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi