loader
Jaji Mkuu ataka mahakama iwepo mipango ya maendeleo

Jaji Mkuu ataka mahakama iwepo mipango ya maendeleo

JAJI Mkuu wa mahakama nchini Prof. Ibrahim Juma amewataka wakuu wa mikoa na wilaya wawe na utamaduni wa kukumbuka na kujumuisha Mahakama katika mipango ya maendeleo, ambayo inafanywa na serikali katika mikoa na wilaya nchini.

Ametoa wito huo wakati akizungumza na wenyeviti wa kamati za mikoa, wenyeviti wa kamati za maadili Wilaya na wajumbe wa kamati hizo katika mkoa wa Mtwara.

"Jambo ambalo mimi huwa napenda kusisitiza ninapokutana na Wakuu wa mikoa na Wilaya ni kuwakumbusha tu kwamba huduma ya utoaji haki ni huduma ya dola ni ya umma pia, tusiwe tunasahau mahakama linapokuja swala la maendeleo," amesema.

Alitaja anuani za makazi Kama huduma mojawapo muhimu ambayo inahitajika na Mahakama katika kujua wanaoleta mashauri wanatoka wapi, kutambua wanaopewa dhamana wanapoishi na viongozi wao.

Alitaja mkongo wa mawasiliano ya taifa na kuwataka wakuu hao wa mikoa na wilaya kuhakikisha kuwa mkongo huo unauganishwa pia kwenye Mahakama zilipo kwenye wilaya na mikoa.

Jaji Mkuu huyo pia amewataka wakuu hao kupeleka na kuunganisha umeme katika Mahakama za mwanzo, ambazo ziko karibu na wananchi pamoja na nyumba za watumishi wa mahakama.

 

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi