loader
Mwenge kuzindua miradi ya Sh bil. 3 Wilaya ya Arusha

Mwenge kuzindua miradi ya Sh bil. 3 Wilaya ya Arusha

MKUU wa Wilaya ya Arusha, Said Mtanda,  amesema Mwenge wa Uhuru umefika leo jijini Arusha na utazindua na kukagua miradi saba yenye thamani ya Sh bilioni 3.4.

DC Mtanda amesema hayo leo jijini Arusha, wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru uliotokea wilayani Monduli na kuingia Jiji la Arusha asubuhi hii.

Amewataka wananchi wa Jiji la Arusha kujitokeza kwa wingi katika miradi mbalimbali inayopitiwa na kusisitiza kuwa mwenge huo unaangaza maendeleo na kuleta manufaa.

Awali Mkurugenzi wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha, Mhandisi Justine Rujomba, anasema mradi huo hadi utakapokamilika utanufaisha wananchi zaidi ya 24,000.

foto
Mwandishi: Veronica Mheta,  Arusha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi