loader
Nyumba za ibada zitumike kukemea ukatili wa watoto

Nyumba za ibada zitumike kukemea ukatili wa watoto

VIONGOZI wa dini wameshauriwa kutumia nyumba za ibada kukemea matendo maovu ikiwemo ukatili wa kijinsia kwa watoto.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa, wakati wa uzinduzi wa mradi wa kupiga vita aina zote za ukatili dhidi ya watoto na vijana.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Tree of Hope Fortunata Manyeresa, amesema mradi huo utafika kata 28 za Jiji hilo na shule 108.

Wadau nao wakatumia fursa hiyo kuiomba serikali kutenga bajeti maalum kwa ajili ya vipimo na  matibabu ya wahanga wa ukatili wa kijinsia, ili kusaidia kumaliza tatizo hilo.

Mratibu wa dawati la jinsia la Jeshi la Polisi Jiji la Tanga, Yasson Mnyanyi, ameeleza kwamba changamoto kubwa ni gharama ya vipimo kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia mara wanapofikishwa katika vituo vya afya na hospitali kubwa.

Inakadiriwa kuwa kwa Jiji la Tanga jumla ya vitendo  vya ukatili 20195 viliripotiwa katika kipindi cha mwaka 2018/19, huku  kesi za ubakaji zikiwa ndio zinaongoza.

foto
Mwandishi: Amina Omari, Tanga

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi