loader
Wafanyabiashara Comoro watembelea Mtwara

Wafanyabiashara Comoro watembelea Mtwara

UJUMBE wa wafanyabiashara kutoka Kisiwa cha Moheli nchini  Comoro, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Chama Cha Wafanyabiashara wa nchi, wametembelea  Taasisi ya Utafiti  wa Kilimo Tanzania (TARI) kituo cha Naliendele kilichopo Mtwara, ili kufahamu na kujionea shughuli mbalimbali za kiutafiti zinazotekelezwa kituoni hapo.

Akizungumza na ujumbe huo ofisini kwake, Mkurugenzi wa Kituo cha TARI Naliendele, Dk. Fortunus Kapinga, alisema kuwa ugeni huo umekuja kuona na kujifunza kibiashara  tafiti mbalimbali na uongezwaji wa thamani wa bidhaa hizo zinazozalishwa na watafiti hao.

Mkurugenzi huyo pia aliwaongoza wageni hao katika kujionea teknolojia kutoka idara mbalimbali pamoja na bidhaa zilizozalishwa kituoni hapo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/10015a2839ef738253c392cdd885945f.jpg

WIZARA ya Afya inaendelea na ...

foto
Mwandishi: Anne Robi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi