WANANCHI mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, wakulima, wajasiriamali, wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya Mkoa wa Katavi pamoja na watumishi wa taasisi za serikali na binafsi wameiomba Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kufanya matembezi ya hiyari kuipongeza serikali ya Awamu ya Sita.
Maombi hayo yametokana na wananchi hao kuguswa na utendaji mzuri wa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wake.
Akizungumza ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, amesema serikali wanaheshimu hisia na matakwa ya wananchi wake, hivyo wanaungana na wananchi katika kutelekeza azma hiyo njema.
Matembezi hayo ya hiyari yanatarajiwa kufanyika Jumamosi Juni 25, 2022 yataanzia Uwanja wa Polisi Buzogwe na kelekea Uwanja wa Kashaulili, ambako matembezi hayo yatapokelewa rasmi.