loader
Tani 15,800 korosho zapelekwa Vietnam

Tani 15,800 korosho zapelekwa Vietnam

KOROSHO tani 15,800 kutoka mkoani Mtwara zimesafirishwa kwenda Vietnam kupitia Bandari ya Mtwara.

Kaimu Maneja wa Bandari ya Mtwara, Robert Kalembwe amesema korosho hizo ni za mwisho kusafirisha nje ya nchi kupitia Bandari ya Mtwara kwa msimu wa 2021/22.

"Kwa upande wa korosho tulikuwa na meli ya mwisho ambayo imeondoka leo asubuhi na imechukua korosho takribani tani 15800 kwenda Vietnam," amesema na kuongeza kuwa meli hiyo ya mwisho ni Kati meli ambazo wamehudumia kwa msimu uliopita wa korosho.

Zaidi ya tani 51, 500 zimesafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia Bandari ya Mtwara.

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho (CBT), Brigedia Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile,  amesema kuondoka kwa meli hiyo kumewapa bodi ya korosho kuendelea kuweka msisitizo kwa ajili ya mavuno ambayo yanatarajiwa kwa msimu ujao.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/2c4c586cc7ebaaa8d13b28b65164cafa.jpg

WIZARA ya Afya inaendelea na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi