WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 23, 2022 atafanya ziara ya siku moja katika Mikoa ya Arusha na Tanga, ambapo atashuhudia awamu ya pili ya wananchi takribani 117 kutoka kaya 27 wanaohama kwa hiari yao wenyewe kutoka eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuelekea Kijiji cha Msomera, Handeni.
Waziri Mkuu pia atakagua makazi na miundombinu ya huduma kwa wananchi katika kijiji cha Msomera, Handeni mkoani Tanga
Pia atakagua alama zilizowekwa kubainisha eneo la hifadhi ya pori tengefu la Loliondo la Kilometa za mraba 1500.
Amewapongeza wakazi hao kwa maamuzi yao ya kuhamia Kijiji cha Msomera, ambapo amewahakikishia Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Samia. Suluhu Hassan ipo pamoja nao.