loader
Mzumbe wafikiria kufungua tawi Tanga

Mzumbe wafikiria kufungua tawi Tanga

CHUO Kikuu Cha Mzumbe kimeonesha nia ya kufungua tawi Mkoa wa Tanga, ili kusogeza huduma za kielimu karibu na wananchi Kanda ya Kaskazini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima mara baada ya kupokea ujumbe wa viongozi wakuu wa chuo hicho kuangalia maeneo ya ardhi, kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya majengo.

Alisema kutokana na mkoa huo kuanza kufunguka kwa fursa mbalimbali za kiuchumi ujio wa chuo hicho, utatoa fursa ya kuwaandaa wananchi wa mkoa huo katika fursa za kiuchumi zilizopo na zinazokuja.

"Nimewaomba kuwepo na vitivo vya mifugo, uchumi wa buluu na masomo mahususi yanayoendana na kanda hii na maeneo mengine kwa ujumla wake,"amesema Malima.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo hicho, Prof. Lughano Kusihika, amesema serikali imeweza kuwapatia mkopo wa masharti nafuu wa  kiasi cha Sh bil 15 Kwa ajili ya maandalizi ya uanzishwaji wa chuo hicho.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/bff12582d8c3594683f4deece411ca84.jpg

MKURUNGENZI wa Kampuni ya Prosperity ...

foto
Mwandishi: Amina Omari,Tanga

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi