loader
Watumia bodaboda kusafirisha meno ya tembo

Watumia bodaboda kusafirisha meno ya tembo

WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majangili sugu wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, baada ya kukutwa na meno ya tembo matano yenye uzito wa kilo 24, wakitumia usafiri wa pikipiki. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Simoni Maigwa, watuhumiwa hao wakiwa katika usafiri wa pikipiki waliyafunga meno hayo katika mfuko wa sandarusi (kiroba) Juni 20, 2022 Kijiji cha Manolo wilayani Lushoto, Tanga.

Taarifa iliwataja waliokamatwa ni pamoja na mzee mwenye umri wa miaka 73 Hassan Shauri, mkulima mkazi wa Kijiji cha Manolo, Eliud Gadi (32), dereva mkazi wa Kijiji cha Manolo na Godson Elikunda (27) dereva, mkazi wa Manolo.

 Amesema kukamatwa watuhumiwa hao ni kunafuatia operesheni iliyofanywa na askari wa ofisi ya Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa wa Kilimanjaro (RCO), kwa kushirikiana na askari wa Shirika Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Taarifa ya Kamanda ilieleza kuwa pikipiki mbili zilikamatwa katika tukio hilo, ambapo namba za usajili ni MC 459 BWQ iliyokuwa ikiendeshwa na Godson Elikuda na nyingine MC 152 CCQ iliyokuwa ikiendeshwa na Eliud Gadi.

 Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda huyo, ilieleza kuwa Gadi akiwa amembeba Hassan Shauri, ambaye ndiye inadaiwa mwenye meno hayo ya tembo.

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Kalist Lazaro amewataka wakazi wa wilaya Lushoto kuacha mara moja kujishughulisha na biashara ya ujangili, kwani vyombo vya ulinzi na usalama katika Mikoa ya Tanga na Kilimanjaro viko macho na vitawasaka wote wenye kufanya biashara hiyo haramu.

‘’Nataka wakazi wote wa Wilaya ya Lushoto kufanya biashara halali yenye kuwaingizia kipato na wale wenye kufanya biashara haramu kwa kutaka utajiri wa haraka hawataachwa salama,’’ alisema Lazaro.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ee1a2d7033c6894f837b8ebe9bca32db.jpg

WIZARA ya Afya inaendelea na ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Moshi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi