loader
Wavamizi maeneo ya mifugo watakiwa waondoke

Wavamizi maeneo ya mifugo watakiwa waondoke

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, sekta ya Mifugo, Tixon Nzunda ameagiza wavamizi katika maeneo ya serikali ya sekta hiyo nchini, waondoke kabla ya kuondolewa na kupata hasara.

Nzunda aliagiza hayo kwenye uzinduzi wa mradi wa uandaaji wa lishe bora na nafuu kwa unenepeshaji ng'ombe Tanzania katika Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania  (Taliri) jijini Tanga.

Alisema maeneo hayo wanayahitaji kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali za malisho, vyakula vya mifugo, uzazi wa mifugo, afya za mifugo na mbari za mifugo.

Alisema wavamizi hao wanadhania kuwa endapo wataondolewa watapata zawadi ya kupewa eneo lingine jambo ambalo halitakuwepo.

" Maeneo haya ni kwa ajili ya kuzalisha mifugo na utafiti," alisema.

 

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi, Tanga

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi