loader
Costech yatoa Milioni 400 mradi kunenepesha Ng'ombe

Costech yatoa Milioni 400 mradi kunenepesha Ng'ombe

TUME ya Sayansi na Teknolojia ( Costech), imetoa zaidi ya sh milioni 400 kwa ajili ya miradi miwili  ikiwa ni uandaaji wa lishe bora ya gharama nafuu kwa unenepeshaji ng'ombe nchini.

Aidha mradi mwingine ni ukarabati wa maabara ya utengenezaji na tathmini ya chakula cha ng'ombe katika taasisi ya utafiti wa mifugo Tanzania ( Taliri), Kanda ya Mashariki kituo cha Tanga.

Mapema leo akizindua mradi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Sekta ya Mifugo Tixon Nzunda aliipongeza Costech kwa ufadhili huo walioutoa kwa Taliri Tanga.

Nzunda amesema mradi huo uliofadhiliwa na Costech lengo lake ni kupata lishe sahihi kwa ajili ya kuongeza ubora wa nyama Tanzania.

Pia ukuzaji na uendelezaji kibiashara teknolojia ya lishe ya unenepeshaji ng'ombe nchini ikiwa ni pamoja na uwezeshaji wa wadau wa tasnia ya nyama nchini.

Awali Meneja Mfuko wa Taifa wa Uendelezaji Sayansi na Teknolojia, Ntufye Mwakigonja amesema kuwa mradi wa maabara umegharimu sh milioni 307 na mradi huo wa uandaaji wa lishe bora umegharimu sh milioni 120.

" Fedha hiyo iliyotolewa kwa Mradi huo wa uandaaji wa lishe bora ya Gharama nafuu kwa Unenepeshaji ng'ombe pia imenunua ng'ombe 30 pamoja na kujenga eneo la majaribio ya Ng'ombe wananenepeshwa kupitia chakula hicho," amesema.

Ameongeza kuwa fedha hizo pia zimetumika kulima ekari 12 za mahindi ambayo yametumika kutengenezea lishe.

" Costech inaigusa sekta ya Mifugo kuzingatia eneo la mapishi kwani mwaka 2020 ilipeleka SUA sh milioni 70 kwa ajili ya kubaini changamoto ya malisho ya Ng'ombe eneo la Ranchi ya Kongwa Dodoma, ambapo malisho yalivamiwa na gugu kongwa," amesema.

Ameongeza kuwa pia Costech ilitoa sh milioni 400 kwa Kituo cha Taliri Mpwapwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taliri Profesa Erick Komba alieleza majukumu ya Taasisi hiyo kuwa ni kusimamia, kuratibu na kufanya tafiti za Mifugo upande wa Tanzania Bara.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8fe9ef618e3b1099597af9f2d6bbb3e5.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi