loader
Costech yaweka nguvu unenepeshaji ng’ombe

Costech yaweka nguvu unenepeshaji ng’ombe

TUME ya Sayansi na Teknolojia (Costech), imetoa zaidi ya Sh milioni 400 kwa ajili ya miradi miwili mojawapo ukiwa ni uandaaji wa lishe bora ya gharama nafuu kwa unenepeshaji ng'ombe nchini.

Akizungumza katika uzindua wa nradi huo wa uandaaji wa lishe bora ya gharama nafuu kwa unenepeshaji ng'ombe nchini, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, sekta ya mifugo Tixon Nzunda aliipongeza Costech kwa ufadhili huo walioutoa kwa Taliri Tanga.

Nzunda amesema mradi huo uliofadhiliwa na Costech lengo lake ni kupata lishe sahihi kwa ajili ya kuongeza ubora wa nyama Tanzania.

Pia ukuzaji na uendelezaji kibiashara teknolojia ya lishe ya unenepeshaji ng'ombe nchini ikiwa ni pamoja na uwezeshaji wa wadau wa tasnia ya nyama nchini.

Kwa Upande wake Meneja Mfuko wa Taifa wa Uendelezaji Sayansi na Teknolojia, Ntufye Mwakigonja, amesema kuwa mradi wa maabara uliogharimu sh milioni 307, na Mradi huo wa uandaaji wa lishe bora sh milioni 120.

Ameongeza kuwa fedha hizo pia zimetumika kulima ekari 12 za mahindi, ambayo yametumika kutengenezea lishe.

 

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/92cbb36849ab2ed9858e11d1006cd12d.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi, Tanga

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi